Umeanza kutumia kompyuta?, je una maswali unaposikia watu
wanasema maneno na misamiati ya kompyuta na ukashindwa kuelewa?, basi makala hii itajadili maada yenye kutambulisha kwako mambo muhimu
yanayohusu kompyuta. Usiwe na hofu, kwa sababu tulipofikia kwa sasa
hatuwezi kukwepa kutumia kompyuta, hivyo ukiwa na uelewa kidogo tu
utakaojifunza hapa, utafahamu kompyuta ni nini na utabaini aina mbalimbali za kompyuta zilizopo.
Haya tuanze kujifunza, Kompyuta ni nini?
Kompyuta ni kifaa cha ki-elektroniki ambacho hufanya kazi kwa kuendesha taarifa, au data. Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua, na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri picha, video na mambo mengine mengi.
Vifaa(Hardware) vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki-elekroniki ambayo inaonekana kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia (Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.
Programu(Software) hazishikiki, ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na kusababisha matokeo ambayo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa programu ni kivinjari cha wavuti (web browser) au programu ya kuandika nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele. Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo hayo.
Chochote unachofanya kwenye kompyuta hutegemea vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hii au nyinginezo. Na baada ya kujifunza aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani vinaweza kutumika kama kipanya.
Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator) ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga (TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.
Tujifunze sasa baadhi ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, maada ya kuelekeza aina zote za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko nje ya makala hii, badala yake tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal computers), kama zifuatavyo.
Hizi utazikuta sana maofisini, majumbani, mashuleni nakadhalika,
zinakaa juu ya meza, zaweza kuwa ndogo, saizi ya kati, au kubwa sana
kimuonekano lakini umbile sio lazima lishabihiane na uwezo, tutakuja
kujifunza sifa zinazoipa uwezo kompyuta kwenye makala nyingine. Mara
nyingi iko pembeni ya Kioo cha kuangalizia (monitor) , pia imeunganishwa
na kipanya (mouse), na kiambaa (keyboard).
Kompyuta ya mezani ni rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu vifaa vyake hutengenezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kiteknolojia sio ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo. Ukilinganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.
Hii ni aina ya pili maarufu ya kompyuta binafsi, ni ndogo na
zinabebeka hivyo waweza kuzitumia karibu kila mahali uendapo kwa sababu
zinatumia betri ya kuchaji. Mara zinatunza chaji kwa muda zaidi ya masaa
mawili, hivyo wengi wanafurahia kuzitumia kwa uhuru wa kuweza kutembea
nazo.
Kutokana na udogo wake sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, lakini huwa zimetengenezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.
Kipanya na kiambaa ni sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo utahitaji.
Kompyuta kibao ni kompyuta ndogo zaidi ya kompyuta mpakato, yenyewe
ni ya kushika mkononi tu, na rahisi zaidi kutembea nayo popote, na huwa
zinakaa na chaji kuliko za kupakata. Badala ya kutumia kipanya na
kiambaa, yenyewe unagusa na vidole vyako kwenye kioo ili kuandika au
kuperuzi, pia zingine huwa na kalamu maalumu (Stylus) unayoweza kuchora
au kuandika juu ya kioo chake. iPad ni mfano wa kompyuta maaarufu ya
namna hii.
Kompyuta hizi, hazifanyi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.
Seva ni kompyuta ambayo inahudumia kompyuta zingine zilizo kwenye
mtandao, mtandao unaweza kuwa wa ndani ya ofisi (local area network), au
mtandao wa wavuti (internet). Makampuni mengi yanatumia seva kuifadhi
mafaili na kutoa huduma zigine kwa wafanyakazi na pia kitoa taarifa kwa
wateja mbalimbali. Seva yaweza kuonekana kama kompyuta ya kawaida
au yenye umbile kubwa zaidi, na kwenye makampuni makubwa seva hutengwa
kwenye vyumba maalumu na hutunzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu
zintegemewa na mamilioni ya wahitajio huduma.
Seva ndio mchezaji mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing). Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya www.youtube.com video zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.
Haya tuanze kujifunza, Kompyuta ni nini?
Kompyuta ni kifaa cha ki-elektroniki ambacho hufanya kazi kwa kuendesha taarifa, au data. Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua, na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri picha, video na mambo mengine mengi.
Vifaa na Programu za Kompyuta.
Kabla hatujajifunza aina za kompyuta, tujifunze vitu/mambo muhimu yanayokamilisha kompyuta. Kompyuta ina sehemu kuu mbili, Vifaa ( Hardware ) na Programu (Software).Vifaa(Hardware) vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki-elekroniki ambayo inaonekana kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia (Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.
Programu(Software) hazishikiki, ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na kusababisha matokeo ambayo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa programu ni kivinjari cha wavuti (web browser) au programu ya kuandika nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele. Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo hayo.
Chochote unachofanya kwenye kompyuta hutegemea vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hii au nyinginezo. Na baada ya kujifunza aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani vinaweza kutumika kama kipanya.
Aina za kompyuta
Wengi wanaposikia kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au kompyuta za mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwishazitaja hapa. Na kwa maendeleo ya teknolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na kila mahali.Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator) ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga (TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.
Tujifunze sasa baadhi ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, maada ya kuelekeza aina zote za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko nje ya makala hii, badala yake tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal computers), kama zifuatavyo.
Kompyuta ya mezani (Desktop Computer)
Kompyuta ya mezani ni rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu vifaa vyake hutengenezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kiteknolojia sio ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo. Ukilinganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.
Kompyuta ya kupakata (Laptop computer)
Kutokana na udogo wake sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, lakini huwa zimetengenezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.
Kipanya na kiambaa ni sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo utahitaji.
Kompyuta Kibao (Tablet computer)
Kompyuta hizi, hazifanyi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.
Seva kompyuta (Server)
Seva ndio mchezaji mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing). Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya www.youtube.com video zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.
Aina nyingine za kompyuta
Kama nilivyogusia awali, leo hii kuna aina lukuki za kompyuta ambazo kwa kiasi kikubwa ni za matumizi maalumu. Ili kuongezea elimu yetu hii, nitaorodhesha baadhi ya kompyuta hizo:-- Simu za mikononi -wengi wanatumia simu za mikononi za kisasa (Smartphones) kufanya mambo mengi ambayo ungeweza kufanya kwenye kompyuta ya mezani kama kucheza michezo (games), kusoma barua pepe, na kuangalia mtandao pia kuwasiliana na marafiki kwenye mitandao ya kijamii
- Kumpyuta za michezo (Game consoles) – mfano playstations n.k, hizi ni kompyuta maalumu kwa michezo ya kwenye luninga, mfano mpira, magari n.k.
- Luninga (TV) – hizi za kisasa zina uwezo wa kuunganisha kwenye mtandao wa wavuti na kufungua taarifa mbalimbali