Sunday, September 4, 2016

KOMPYUTA NI NINI?

Umeanza kutumia kompyuta?, je una maswali unaposikia watu wanasema maneno na misamiati ya kompyuta na ukashindwa kuelewa?, basi  makala hii itajadili maada yenye kutambulisha kwako mambo muhimu yanayohusu kompyuta. Usiwe na hofu, kwa sababu tulipofikia kwa sasa hatuwezi kukwepa kutumia kompyuta, hivyo ukiwa na uelewa kidogo tu utakaojifunza hapa, utafahamu kompyuta ni nini na utabaini aina mbalimbali za kompyuta zilizopo.

Haya tuanze kujifunza, Kompyuta ni nini?
Kompyuta ni kifaa cha ki-elektroniki ambacho hufanya kazi kwa kuendesha taarifa, au data. Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua, na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri picha, video na mambo mengine mengi.

Vifaa na Programu za Kompyuta.

Kabla hatujajifunza aina za kompyuta, tujifunze vitu/mambo muhimu yanayokamilisha kompyuta. Kompyuta ina sehemu kuu mbili, Vifaa ( Hardware ) na Programu (Software).
Vifaa(Hardware) vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki-elekroniki ambayo inaonekana kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia (Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.
Programu(Software) hazishikiki, ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na kusababisha matokeo ambayo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa programu ni kivinjari cha wavuti  (web browser) au programu ya kuandika nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele. Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo hayo.
Chochote unachofanya kwenye kompyuta hutegemea vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hii au nyinginezo. Na baada ya kujifunza aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani vinaweza kutumika kama kipanya.

Aina za kompyuta

Wengi wanaposikia kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au kompyuta za mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwishazitaja hapa. Na kwa maendeleo ya teknolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na kila mahali.
Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator) ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga (TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.
Tujifunze sasa baadhi ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, maada ya kuelekeza aina zote za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko nje ya makala hii, badala yake tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal computers), kama zifuatavyo.

Kompyuta ya mezani (Desktop Computer)


Hizi utazikuta sana maofisini, majumbani, mashuleni nakadhalika, zinakaa juu ya meza, zaweza kuwa ndogo, saizi ya kati, au kubwa sana kimuonekano lakini umbile sio lazima lishabihiane na uwezo, tutakuja kujifunza sifa zinazoipa uwezo kompyuta kwenye makala nyingine. Mara nyingi iko pembeni ya Kioo cha kuangalizia (monitor) , pia imeunganishwa na kipanya (mouse), na kiambaa (keyboard).
Kompyuta ya mezani ni rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu vifaa vyake hutengenezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kiteknolojia sio ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo. Ukilinganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.

Kompyuta ya kupakata (Laptop computer)


Hii ni aina ya pili maarufu ya kompyuta binafsi, ni ndogo na zinabebeka hivyo waweza kuzitumia karibu kila mahali uendapo kwa sababu zinatumia betri ya kuchaji. Mara zinatunza chaji kwa muda zaidi ya masaa mawili, hivyo wengi wanafurahia kuzitumia kwa uhuru wa kuweza kutembea nazo.
Kutokana na udogo wake sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, lakini huwa zimetengenezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.
Kipanya na kiambaa ni sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo utahitaji.

Kompyuta Kibao (Tablet computer)


Kompyuta kibao ni kompyuta ndogo zaidi ya kompyuta mpakato, yenyewe ni ya kushika mkononi tu, na rahisi zaidi kutembea nayo popote, na huwa zinakaa na chaji kuliko za kupakata. Badala ya kutumia kipanya na kiambaa, yenyewe unagusa na vidole vyako kwenye kioo ili kuandika au kuperuzi, pia zingine huwa na kalamu maalumu (Stylus) unayoweza kuchora au kuandika juu ya kioo chake. iPad ni mfano wa kompyuta maaarufu ya namna hii.
Kompyuta hizi, hazifanyi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.

Seva kompyuta (Server)


Seva ni kompyuta ambayo inahudumia kompyuta zingine zilizo kwenye mtandao, mtandao unaweza kuwa wa ndani ya ofisi (local area network), au mtandao wa wavuti (internet). Makampuni mengi yanatumia seva kuifadhi mafaili na kutoa huduma zigine kwa wafanyakazi na pia kitoa taarifa kwa wateja mbalimbali. Seva yaweza kuonekana kama kompyuta ya kawaida au yenye umbile kubwa zaidi, na kwenye makampuni makubwa seva hutengwa kwenye vyumba maalumu na hutunzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu zintegemewa na mamilioni ya wahitajio huduma.
Seva ndio mchezaji mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing). Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya www.youtube.com video zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.


Aina nyingine za kompyuta

Kama nilivyogusia awali, leo hii kuna aina lukuki za kompyuta ambazo kwa kiasi kikubwa ni za matumizi maalumu. Ili kuongezea elimu yetu hii, nitaorodhesha baadhi ya kompyuta hizo:-
  1. Simu za mikononi -wengi wanatumia simu za mikononi za kisasa (Smartphones) kufanya mambo mengi ambayo ungeweza kufanya kwenye kompyuta ya mezani kama kucheza michezo (games), kusoma barua pepe, na kuangalia mtandao pia kuwasiliana na marafiki kwenye mitandao ya kijamii
  2. Kumpyuta za michezo (Game consoles) – mfano playstations n.k, hizi ni kompyuta maalumu kwa michezo ya kwenye luninga, mfano mpira, magari n.k.
  3. Luninga (TV) – hizi za kisasa zina uwezo wa kuunganisha kwenye mtandao wa wavuti na kufungua taarifa mbalimbali


Hitimisho

Tumejifunza kompyuta ni nini?, na watu hutumia kompyuta kufanya mambo gani, pia tumeona baadhi ya aina mbalimbali za kompyuta na kufahamu matumizi yake na mipaka yake kwa ujumla. Somo hili halitaishia hapa kwani bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kompyuta hizi, kwenye makala nyingine tutajifunza kuhusu uwezo wa kompyuta na unaweza vipi kufahamu, pia sifa za programu endeshi za kompyuta hizo.

Tafadhali endela kufungua tovuti hii ili uweze kujifunza zaidi kuhusu mambo ya TEHAMA.

Monday, August 8, 2016

VIJUE VIFAA VYA KOMPYUTA






PICHA ZA KOMPYUTA NA VIFAA MBALIMBALI ZA VITU VINAVYOHUSIANA NA KOMPYUTA.


Kuna aina mbalimbali za kompyuta na ambazo zina maumbo na miundo tofautitofauti.

Hapa chini kuna aina mbali mbali za picha zinazoonyesha aina mbalimbali za kompyuta hizo.


Kompyuta hizi hapa ndiyo aina mabyo watu wengi wamezoea kuziona na kuzitumia.

Hii huitwa Deski topu kompyuta/Desktop Computer.




Hii kompyuta ndogo inaitwa laputopu/laptop. Ni aina ndogo ambayo hufaa kubeba na kutembea nayo sehemu mbalimbali. 



Vifaa Vikuu

Kuna aina kuu tano za vifaa vumikavyo katika kompyuta:

  1. Vifaa vya kuingiza:
    [input devices]

    Vifaa vya kuingiza ni vifaa atumiavyo mtumiaji kuwasiliana/kuongea na kompyuta unayotumia.Hapa chini kuna picha na maelezo mafupi juu ya vifaa hivyo;

    (1): Kiibodi [keyboard]:

    Hiki ni kifaa kitumikacho kwa kuandikia. Kupitia hiki kifaa mtumiaji huweza kupata herufi zote na namba kwa mpangilio wa kiitaalamu ambao humfanya aweze kuandika kazi zake

  2. Pia kuna baadhi ya vitufe muhimu ambavyo inapaswa mtumiaji wa kompyuta anapaswa avifahamu ili kuweza kuafanya kazi yake bila mkwaruzo.
      1. Cha kwanza ni SPACE-BAR hiki kinapatika kwenye kiibodi yako kwenye vitufe vya upande katikati juu . Hiki kitufe kazi yake ni kufuta kwa hatua kwa kurudi nyuma.


      2. Upande wako wa kushoto kwenye vitufe vilivyoko mwishoni kuna kitufe kingine kilichoandikwa CAPS LOCK .

        Hiki kitufe kazi yake ni kubadilisha maandishi toka herufi ndogo kwenda kwenye herufi kubwa na kinyume chake.


      3. Kitufe kingine ni kile kilichopo upande wa kushoto pia chini ya kile cha caps lock . Hiki kinaitwa SHIFT

        hiki kinweza kutumika pia kubadilisha herufi kubwa na ndogo vilevile ila unapaswa kukishikilia wakati unapobadilisha. Shift zipo mbili moja upande wa kushoto na nyingine katikati ila zote zinafanya kazi sawa.


      4. Upande wa katikati kuna kitufe kingine kinachoitwa DELETE

        hiki kazi yake ni kufuta maandishi yote yale ambayo utakuwa umeyachagua.


      5. Sehemu ya kati ya kiibodi yako pamoja na upande wa kulia wa kiibodi yako chini kuna vitufe vilivyoandikwa ENTER.

        Hivi vitufe kazi yake kubwa ni kubadilisha toka aya moja kwenda nyingine na pia hutumika kusogeza ukurasa au aya chini pale unapokibonyeza huku kasa ikiwa ipo kwenye aya hiyo.

        Kwa upande mwingine hutumika kukubali yaani pale unapotakiwa kutekeleza agizo au maelekezo fulani ukibonyeza kitufe hiki humaanisha ndiyo yani umekubali au umesema sawa kwa kile unachoulizwa.


    (2): Mausi/kiongozeo [Mouse]:

  3. Mausi ni chombo muhimu katika kompyuta ambacho hutuongoza na kutuonesha mahali tutakapoandika au kufanyia kitu chochote kwenye ukurasa tulio ufungua, hapa chini kuna maelezo ya matumizi yake kwa kina;

    Namna ya Kutumia Mausi/kiongozeo chako:
    [ How to use Your Mouse]:

    1. Kunavitufe viwili kwenye kila mausi/kionesheo. Ila kompyuta aina ya Apple inakuwa na kimoja tu na ambacho hutumika kama hizi nyingine kwa kubonyeza upande wa kushoto na kulia.

    2. Kitufe cha upande wa kushoto kwenye mausi/kiongozeo hutumika kufungulia programu na kuchagulia (to select items) maandishi au maneno au picha kwa ajili ya kuikopi, kukata au vinginevyo

    3. Kitufe cha upande wa kushoto hutumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kufanya.


    Kasa






    (3):Kipaza sauti: [Microphone]:


    Hiki katika kompyuta kurekodi sauti kwa ajili ya kuituma kama barua pepe au simu.

    (4):Skana/Scanner


    Hiki hutumika kubadili picha kutoka katika hali ya kawaida na kuinakili na kuifanya iwe katika mfumo wa kielektroniki na kuweza kutumwa kwa pamoja na barua pepe na pia kuweza kuhifadhiwa na kuonekana kwenye mdahalishi.

  4. Vifaa vya uendeshaji: [processing devices]:

    Sakiti/Circuit



    Hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho Central Processing Unit (C.P.U.). Mfano wake ni sakiti circuit; hiki huendesha na na kuunganisha pamoja habari na taarifa zote kwenye kompyuta.
  5. Vifaa vya Kuhifadhia/kuhifadhia [Storage devices]

    Vifaa hivi hutumiwa kwenye kompyuta kuhifadhi na kukumbuka habari mbalimbali

    (1): Flopi diski draivu/ Floppy disk drive (mara nyingi hujulikana kama A: draivu)



    Diski draivu hutumika kuingizia disketi ilkuhifadhia data au kazi za mtumiaji.

    Disketi ni kifaa kinachoondosheka/kubebeka na ambacho hutumiwa kunakilia na kuhifadhia data na kazi mbalimbali za watumiaji wa kompyuta.

    (2): CD Rom draivu /CD Rom disk drive.


    Hizi zina ni sehemu zinayotunza kumbukumbu za data mbalimbali (Memory).

    (3):Hadi diski Draivu/Hard Disk Drive

    Hii hujulikana zaidi kwa jina la Draivu "C" na kuwa inapatikana ndani ya kompyuta.

  6. Vifaa vya kutoa: [Output devices]

    (1):Skrini/kioo: [screen/monitor]:

    Hiki ni kioo cha kompyuta ambacho ndicho mtumiajia anachoangalia na kuyaona yale yote ambayo anayafanya kwa kutumia kompyuta yake.



    (2):Kichapishio: [printer]:

    Hiki hutumika kuchapishia kazi mbalimbali kutoka katika kompyuta.

    (3):Spika: [Speakers]:

    Hizi spika hutumika kusililizia muziki, maelezo na sauti mbalimbali toka kwenye kompyuta

    .

  7. Vifaa vya kuwasiliana [Communication Devices]



    (1): Kebo: [Cables]:

    Kebo hutumika kuunganishia kopyuta na vifaa vingine kwenye umeme



(2): Modemu: [Modem]:

Modemu hupatikana ndani ya kompyuta japo zamani zilikuwa nje ya kompyuta . Hii hutumika kuunganishia kompyuta kwenye mtandao wa mdahalishi.

MAFUNZO YA COMPUTER

SUMSUNG COMPUTER

COMPUTER YA MEZANI/DESK TOP

ORODHA YA LAPTOP 10 BORA




 Watu wengi huingia madukani kila mara kununua computer. Yaweza kuwa Desktop au laptop kulingana na mahitaji yako. Kuna baadhi ya watu huniuliza swali hili, ninataka kununua laptop, unanishauri nichukue laptop gani?


 Unapohitaji kununua computer hasa laptop, kwanza kuwa makini na nini ungependa kufanya kwa kutumia laptop hiyo. Kama wewe ni mtaalamu wa masuala ya computer kwa shughuli nzito kama kudesign picha, video, beats lazima unahitaji computer yenye RAM kubwa(angalau 3GB) , video card kubwa, yenye hard disk(angalau 350GB) kubwa pia. Kwa matumizi ya nyumbani tu sio lazima iwe na RAM kubwa (2GB inatosha) au processor(1.5GHz inatosha) bali hard disk inabidi iwe na uwezo wa kutosha (Angalau 250GB).

Basi tusifanye mambo yawe marefu. Leo nitakutajia laptop 10, bora zaidi sokoni kwa sasa. Takwimu hizi zimekusanywa na watumiaji wengi wa computer duniani. Gharama na ubora wa laptop huenda sambamba. Lakini kumbuka kuwa kampuni iliyotengeneza laptop fulani sio lazima tu kila laptop yao inakidhi matakwa yako, zingatia Hard disk size, RAM, processor, video na graphics card, ukubwa na uzito pia ubora wa betri.

1. NANI ZAIDI YA APPLE!?

Niamini hakuna zaidi. Laptop za Apple, Macbook Air ndizo bora zaidi sokoni. Laptop hizi hutengenezwa kwa aluminium.Hutumia SSD ambazo zina kasi kama mara 4 zaidi ya Hard disk za kawaida. Zaidi Operating system yake ni safi na ya kipekee isiyoshambuliwa na virusi. Sababu kubwa ambayo huwafanya watu wasiwe na laptop hizi hasa hapa Afrika mashariki ni bei zake ghali.







2. Hewlett-Packard (HP)


Ubora: 4.5/5
Watumiaji:1/5

Huweza kukaa kwa muda mrefu. Ni ngumu, ni bora, ni bei NZURI. HP ni kampuni kongwe zaidi kupita Dell na wengine. Laptop zao ndizo zinazoaminika zaidi, ni bora zaidi na bado bei zake ni nzuri zaidi. Hii ndiyo laptop bora inayotumia platform kama Windows.






3. Dell. 

Ubora: 4/5
Watumiaji: 3/5

Zina warranty ya muda mrefu kupita computer zote sokoni. Dell huwa na speaker zinazotoa mziki mzuri. Pia uwezo wa screen zake ni mzuri sana. Ni bora kwa matumizi ya nyumbani na ofisini. Zina nguvu kubwa sana. Computer mpya za Dell Alienware ndizo laptop zenye nguvu zaidi kupita computer zote kwa sasa.

4. Asus.






Ubora: 4/5
Watumiaji: 0.5/5

Motherboard au ramani ni muhimu kwa kifaa chochote cha elektroniki. Asus ni kampuni inayokubalika kwa kutengeneza motherboard ambazo pia hutumiwa na makampuni mengine kama Dell, Acer na Lenovo. Hivyo basi lazima wao weyewe computer zao ziwe bora kwa akili ya kawaida tu. Asus hutengeneza laptop bora. Hupata Errors chache zaidi kama unatumia platform za windows na Ubuntu.






5. Acer

Ubora: 4/5      Watumiaji: 3/5

Kama unazungumzia laptop za kisasa hautaiacha acer. Kweli laptop hii ni bora  na ingestahili kuwa juu kabisa katika list hii kama isingekuwa ghali kidogo. Ina nguvu kubwa ya kufanya kazi na graphics pamoja na video. Acer zilizo na touch screen zinasemekana kuwa nzuri zaidi ya laptop nyingine zenye touch screen. Betri za acer pia ni bora kwa mujibu wa maoni mbalimbali ya watumiaji wake.

Listi ya 5 zilizobaki ni kama hii hapa chini.
6. Lenovo
7. Toshiba
8. Samsung
Ni ngumu kuamini kama kweli hii ndiyo nafasi ya samsung katika kumi hizi bora zaidi. Samsung ni moja kati makampuni bora zaidi ya elektroniki duniani. Hutengeneza bidhaa nyingi na bora. Uwezekano wa idadi kubwa ya watu kutumia laptop zao uko chini kupita jinsi watu wanavyoamini simu zao. Laptop za samsung zimekuwa zikipata hitilafu mara nyingi zaidi ya hizo nyingine. Hata hivyo laptop hizi ni poa zaidi, si unajua tena, made in Seoul, China.


9. Alienware
10.Sony.

COMPUTER AINA YA HP

COMPUTER AINA YA DELL

Tofauti kati ya Blog. Websites na Applications

 
1. Kwanza elewa neno WEB ni nini:
WEB ni kifupisho cha neno zima WORLD WIDE WEB - si umeona websites nyingine zinaanza na www, basi www ni kifupisho cha World Wide Web. Kwa lugha rahisi WEB ni namna maalum ya ku share taarifa kupitia internet kwa kuunganisha mawasiliano toka kompyuta tofauti tofauti ulimwenguni. Kama vile mie nipo nchini Colombia naandika maneno haya kwa laptop yangu wewe hapo ulipo unasoma hii post kwa- sababu ya hii teknolojia ya world wide web (web).
2.WEBSITE ni muunganisho wa maneno mawili WEB na SITE.
Wajua neno web nini , basi unganisha na neno SITE kama unavyojua neno SITE ni eneo maalum kwa ajili ya shughuli maalum, au sio ? Basi WEBSITE inamaanisha ni sehemu maalum ambapo habari au taarifa fulani zinapatikana. Mfano kama wataka kusoma status za rafiki zako wa FB basi wajua ni lazima uende FACEBOOK. Hivyo FACEBOOK ni SITE kwako maalum kwa  kucheki mambo maalum kama hayo ya status ! Kwakuwa FB ni site iliyopo ndani ya muunganiko tuuitao WEB, hivyo FB tunaiita WEBSITE.
3. Kwa mujibu wa Wikipedia, neno blog ni kifupisho cha neno Web LOG, yaani rekodi au usajili wa taarifa za mara kwa mara ndani ya WEB. Ili kufupisha neno zima WEB BLOG wakaita kwa kifupi BLOG-yaani kutoka neno WEB, tumechukua herufi B, halafu tukaunganisha na neno LOG, hivyo kuwa na BLOG.
--Kuelewa utafauti kati ya BLOG na WEBSITE kunategemea sana kuelewa hayo maneno matatu hapo juu yaani WEB,  WEBSITE na BLOG. 
Zifuatazo ni tofauti kati ya blog na website:-
Uandishi :  Kwenye blogs tuna kitu tunaita POSTS ambapo hayo ni maelezo yanayowekwa na mwandishi wa blog mara kwa mara. Hata hivyo websites kwa asili huwa hazibadilishwi taarifa mara kwa mara kama ilivyo blog. 
Uhifadhi wa taarifa: Blogs zina mtindo maalum wa kuhifadhi posts toka ya kwanza mpaka ya mwisho kuiandika. Na mara nyingi waweza kuona hifadhi (ARCHIVE) ya posts hizo katika blogs nyingi, hata hivyo websites  nyingi huwa hazina hifadhi ya taarifa zao za siku za nyuma ndani ya websites husika.
Teknolojia: Mtu yoyote yupo huru kuandaa website kwa mtindo anaotaka yeye, tofauti na blogs ambapo tayari teknolojia yake inategemeana na matakwa ya kampuni husika inayotoa huduma ya blogging. Mfano kuna wordpress inao mtindo wake maalum, na blogger nao wana mtindo wao maalum wa jinsi blogs zao zitakavyotokea au jinsi utakavyoziandaa.
Ushirikishwaji wa wasomaji:  Mara nyingi kwenye blogs huwa tuna sehemu ya comments kwa kila post, wakati taarifa za websites nyingi hazina kipengele cha ku comment.


 ANGALIZO:  Asasi  nyingi siku hizi zimekuwa zikiambatanisha teknolojia ya blog katika websites zao ili kuendelea kuwa karibu na wateja wao watarajiwa.

Maana ya RAM , HARD DISK na PROCESSOR kama zitumikavyo katika COMPUTER

RAM ikiwa ni kifupisho cha neno Random Access Memory ni aina ya uhifadhi kumbukumbu utumikao na kompyuta kuhifadhi kumbukumbu kwa muda mfupi tu.

Kompyuta inapozimwa au programu ikifungwa basi RAM nayo huipoteza kumbukumbu hiyo wakati huo huo.

Kama ilivyo nyenzo yoyote, RAM huwa na utofauti wa kuhifadhi kumbukumbu yaani zipo zenye memory kubwa na ndogo, pia hutofautiana speed yaani uwezo wa kuprocess data etc


HDD ikiwa ni kifupisho cha Hard Disk Drive ni kifaa kitumiwacho na kompyuta kuhifadhi operating system, programu pamoja na makabrasha yote yatumiwayo ama na kompyuta au mtumiaji kompyuta.


Kinachohifadhiwa katika HDD huendelea kuwepo hata kama kompyuta imezimwa, kabrasha limefutwa n.k, kumbukumbu hii ni ya kudumu.

Kama ilivyo kwa RAM, HDD nayo huwa na sifa ya kuwa na memory size, processing speed etc


Processor ni sehemu ya kompyuta ambayo inahusika na ukokotozi, uendeshaji na uchakataji wa kila jambo linaloendelea katika kompyuta. Kwa kifupi humithilishwa na ubongo wa wanadamu.

Sidhani kama kuna jibu la moja kwa moja juu ya aina za processor.

Kuna utofauti wa kikampuni, utendaji, ufanisi, matoleo n.k
(Cache, clock speed, host bus speed etc)