1. Kwanza elewa neno WEB ni nini:
WEB ni kifupisho cha neno zima WORLD WIDE WEB - si umeona websites
nyingine zinaanza na www, basi www ni kifupisho cha World Wide Web. Kwa
lugha rahisi WEB ni namna maalum ya ku share taarifa kupitia internet
kwa kuunganisha mawasiliano toka kompyuta tofauti tofauti ulimwenguni.
Kama vile mie nipo nchini Colombia naandika maneno haya kwa laptop yangu
wewe hapo ulipo unasoma hii post kwa- sababu ya hii teknolojia ya world
wide web (web).
2.WEBSITE ni muunganisho wa maneno mawili WEB na SITE.
Wajua neno web nini , basi unganisha na neno SITE kama unavyojua neno
SITE ni eneo maalum kwa ajili ya shughuli maalum, au sio ? Basi WEBSITE
inamaanisha ni sehemu maalum ambapo habari au taarifa fulani
zinapatikana. Mfano kama wataka kusoma status za rafiki zako wa FB basi
wajua ni lazima uende FACEBOOK. Hivyo FACEBOOK ni SITE kwako maalum kwa
kucheki mambo maalum kama hayo ya status ! Kwakuwa FB ni site iliyopo
ndani ya muunganiko tuuitao WEB, hivyo FB tunaiita WEBSITE.
3. Kwa mujibu wa Wikipedia, neno blog ni kifupisho cha neno Web LOG,
yaani rekodi au usajili wa taarifa za mara kwa mara ndani ya WEB. Ili
kufupisha neno zima WEB BLOG wakaita kwa kifupi BLOG-yaani kutoka neno
WEB, tumechukua herufi B, halafu tukaunganisha na neno LOG, hivyo kuwa
na BLOG.
--Kuelewa utafauti kati ya BLOG na WEBSITE kunategemea sana kuelewa hayo maneno matatu hapo juu yaani WEB, WEBSITE na BLOG.
Zifuatazo ni tofauti kati ya blog na website:-
Uandishi : Kwenye blogs tuna kitu tunaita POSTS ambapo hayo ni maelezo
yanayowekwa na mwandishi wa blog mara kwa mara. Hata hivyo websites kwa
asili huwa hazibadilishwi taarifa mara kwa mara kama ilivyo blog.
Uhifadhi wa taarifa: Blogs zina mtindo maalum wa kuhifadhi posts toka ya
kwanza mpaka ya mwisho kuiandika. Na mara nyingi waweza kuona hifadhi
(ARCHIVE) ya posts hizo katika blogs nyingi, hata hivyo websites nyingi
huwa hazina hifadhi ya taarifa zao za siku za nyuma ndani ya websites
husika.
Teknolojia: Mtu yoyote yupo huru kuandaa website kwa mtindo anaotaka
yeye, tofauti na blogs ambapo tayari teknolojia yake inategemeana na
matakwa ya kampuni husika inayotoa huduma ya blogging. Mfano kuna
wordpress inao mtindo wake maalum, na blogger nao wana mtindo wao maalum
wa jinsi blogs zao zitakavyotokea au jinsi utakavyoziandaa.
Ushirikishwaji wa wasomaji: Mara nyingi kwenye blogs huwa tuna sehemu
ya comments kwa kila post, wakati taarifa za websites nyingi hazina
kipengele cha ku comment.
ANGALIZO: Asasi nyingi siku hizi zimekuwa zikiambatanisha teknolojia
ya blog katika websites zao ili kuendelea kuwa karibu na wateja wao
watarajiwa.
No comments:
Post a Comment